WANAFUNZI 32,957 KUFANYA MTIHANI WA KITAIFA WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2026 MKOA WA ARUSHA 🇹🇿 - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 19 October 2026

WANAFUNZI 32,957 KUFANYA MTIHANI WA KITAIFA WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2026 MKOA WA ARUSHA 🇹🇿

 


Mwandishi Maalumu  RS  Arusha


maipacarusha20@gmail.com 


Jumla ya wanafunzi 32, 957 mkoa wa Arusha wanatarajiwa Mtihani Upimaji wa Taifa wa Kidato cha nne mwaka 2026 mkoa wa Arusha kwa mujibu wa mabadiliko ya ratiba iliyotolewa na Baraza la Mitihani la Taifa - NECTA, kwa mwaka 2026.


Katibu Tawala Msaidizi Idara ya Elimu Mkoa wa Arusha, Mwl. Dkt.Vicent Kayombo amesema kuwa, kati ya wanafunzi hao 32, 957 waliosajiliwa kufanya mtihani huo wa Taifa mwaka 2026,  wavulana ni 15,087 sawa na asilimia 45.8 na wasichana ni 17,870 sawa na asilimia 54.2 huku watainiwa wa binafsi ni 513 wavulana 253 na wasichana 513.


Amefafanua kuwa, idadi hiyo ya wanafunzi waliosajiliwa ni sawa na asilimia 84.9 ya wanafunzi 38, 826 waliondikishwa kuanza kidato cha kwanza mwaka 2023,  huku jumla ya shule za Sekondari 280 zikiwa na vitua vya kufanyia mitihani, ambapo shule 180 za Serikali sawa na asilimia 64.3 na shule 100 za binafsi sawa na asilimia 35.7. 


"Mitihani hiyo itafanyika kuanzia Oktoba  19 hadi Novemba 06, 2026, kwa mujibu wa Sheria, taratibu na Kanuni za Mitihani ya Taifa, maandalizi yote yamekamilika  ikiwa ni pamoja kufanyika kwa semina elekezi kwa  wasimamizi wote wa mitihani lakini pia maandaliwa ya  watahiniwa yamekamilika, watahinjwa wameandaliwa vema kitaaluma, kiakili na kisaikolojia, aidha ninawatakia kila la kheri katika mtihani wao wa Taifa ". Amebainisha Dkt.Kayombo


Aidha, ametoa wito kwa watahiniwa wote kuwa  watulivu, kujiamini na kumtanguliza Mwenyenzi Mungu wakati wote mitihani pamoja na kuwasisitiza wasimamizi wa mitihani hiyo kuzingatia taratibu za mitihani ya Taifa kwa kujiepusha na vitendo vilivyo kinyume na taratibu hizo huku akiwataka kutambua kuwa Serikali imewapa dhamana kubwa iliyobeba hatma ya maisha ya wanafunzi wanaowasimamia.


Awali, Dkt.Kayombo amewatakia wanafunzi wote mtihani mwema pamoja na kuwaombea kwa Mwenyenzi Mungu wapate ufaulu mzuri na hatimaye kufikia ndoto zao kwa kuwa Taifa la Tanzania linawategemea kuwa watalamu baadaye.

No comments: