KAIZER JOHN JEOFFREY KUIACHA TRA UNITED, KUELEKEA ITALIA. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday, 27 November 2026

KAIZER JOHN JEOFFREY KUIACHA TRA UNITED, KUELEKEA ITALIA.

 

 

Mlinda mlango wa TRA United SC, Kaizer John Jeoffrey


Mwandishi Wetu


maipacarusha20@gmail.com 


Mlinda mlango wa TRA United SC, Kaizer John Jeoffrey, anatajwa kuwa mbioni kujiunga na klabu ya A.C. Legnano 1913 inayoshiriki michuano ya soka nchini Italia. 


Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, mazungumzo kati ya pande hizo mbili yamefikia hatua nzuri, huku mlinda mlango huyo akitarajiwa kusafiri kuelekea Italia kwa ajili ya kuanza safari mpya ya kisoka endapo taratibu za usajili zitakamilika.


Hatua hiyo inaelezwa kuwa fursa muhimu kwa Jeoffrey kupata changamoto mpya nje ya Tanzania na kujitangaza katika soka la kimataifa.


Uwezekano wa kujiunga na A.C.Legnano unaweza kuwa mwanzo wa ukurasa mpya katika maisha yake ya soka, huku akitarajiwa kukutana na mazingira tofauti ya ushindani na maendeleo ya mchezo huo barani Ulaya.


Jeoffrey, ambaye amekuwa sehemu ya kikosi cha TRA United SC, anatajwa kuwa miongoni mwa makipa wanaopata fursa ya kutafuta mafanikio nje ya mipaka ya Tanzania akiwa ni mchezaji huru kwa Sasa. 


Endapo dili hilo litakamilika rasmi, hatua hiyo itaongeza idadi ya wachezaji wa Kitanzania wanaopata nafasi ya kuonyesha uwezo wao katika klabu za nje ya nchi.


No comments: