Rais Samia ahimiza matumizi ya nishati safi ya kupikia shule, hospitali - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 12 November 2026

Rais Samia ahimiza matumizi ya nishati safi ya kupikia shule, hospitali

 





Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amehimiza matumizi ya nishati safi ya kupikia katika shule, hospitali na taasisi nyingine za umma akieleza kuwa matumizi ya nishati zisizo safi yanaongeza gharama za uendeshaji, kuhatarisha afya za watumiaji na kusababisha athari kwa mazingira.


Amesema taasisi zinazotegemea njia za jadi za kupikia kama kuni na mkaa zinakabiliwa na mazingira yasiyo rafiki ya kazi kutokana na moshi unaotokana na nishati hizo, hali inayoweza kuathiri afya za wapishi na watu wengine wanaotumia mazingira hayo.


Akizungumza katika tukio la ngazi ya juu kuhusu kuendeleza mageuzi ya sekta ya nishati Tanzania na matumizi ya nishati safi ya kupikia katika shule na taasisi za afya, lililofanyika pembezoni mwa Mkutano wa 31 wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31) jijini Antalya, Uturuki, Rais Samia amesema Serikali imeweka matumizi ya nishati safi ya kupikia kuwa sehemu muhimu ya ajenda ya mageuzi ya sekta ya nishati nchini.


Amesema kupitia Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia wa mwaka 2024/34, Serikali inalenga kuhakikisha angalau asilimia 80 ya Watanzania wanapata suluhisho za nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.


Lengo hilo linahusisha kuongeza matumizi ya teknolojia na vyanzo vya nishati safi ili kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa, kulinda afya za wananchi na kupunguza athari za kimazingira. #TanzaniaCOP31

No comments: