Mwandishi wetu
maipacarusha20@gmail.com
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, amemkabidhi rasmi nyenzo mbalimbali za kazi Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Angellah Kairuki, ikiwa ni sehemu ya makabidhiano ya majukumu ya uongozi wa Wizara hiyo. Makabidhiano hayo yamefanyika kwa lengo la kuhakikisha uendelevu wa shughuli za Wizara pamoja na kuwezesha uongozi mpya kupata nyaraka na taarifa muhimu zinazohusu utekelezaji wa majukumu yake.
Makabidhiano hayo yamefanyika Novemba 27, 2026 jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya Viongozi hao kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Nyenzo hizo ikiwemo taarifa mbalimbali, zitamwezesha Mhe. Kairuki kuendelea kusimamia na kuratibu masuala ya ushirikiano wa kikanda, hususan utekelezaji wa majukumu ya Tanzania ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Mhe. Angellah Kairuki anatarajiwa kuendeleza usimamizi na uratibu wa masuala ya Mtangamano wa Kikanda kupitia Jumuiya ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), hatua inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kuhakikisha Tanzania inaendelea kunufaika na fursa zinazotokana na Jumuiya hiyo.

No comments:
Post a Comment