OLE MILLYA AJITOSA KUGOMBEA UJUMBE WA HALMASHAURI KUU CCM MKOA WA ARUSHA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 23 March 2023

OLE MILLYA AJITOSA KUGOMBEA UJUMBE WA HALMASHAURI KUU CCM MKOA WA ARUSHA

 

James Olle Millya akionesha fomu ya kugombea ujumbe wa halmashauri kuu CCM Mkoa wa Arusha kwa waandishi wa Habari mara baada ya kuchukua fomu hiyo mapema leo katika ofisi za CCM Mkoa wa Arusha.

NA:ANDREA NGOBOLE, ARUSHA

maipacarusha20@gmail.com

 

Harakati za kugombea ujumbe wa halmashauri kuu wa chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha zimeanza kwa Vigogo wa chama hicho kujitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo nyeti kwa chama tawala nchini Tanzania.


Fomu hizo zimeanza kuchukuliwa leo March 23 na wanachama wa chama hicho  ambapo mwanachama wa kwanza kujitokeza  kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo ni Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) James ole Millya.

 

Wakili Olle Millya akionesha Fomu ya    kugombea ujumbe wa NEC CCM mara baada ya kuchukua fomu katika ofisi ya Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha

 


Olle Millya ambaye kwa sasa ni mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Africa MAshariki (EALA) anasema  ana uzoefu wa muda mrefu na siasa za mkoa wa Arusha ambazo zinahitaji vijana imara kama yeye kuwezesha kushinda majimnbo ya mkoa huo kwani amekuwa mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha na mbunge wa jimbo la Simanjiro hivyo ameona ni vema agombee nafasi hiyo ili kuusaidia Mkoa wa Arusha ambao una joto kubwa la kisiasa, hivyo ni lazima timu imara iwepo kuhakikisha chaguzi zijazo chama hicho kinashinda kwa kishindo .


Alisema yeye kama kijana aliyepikwa na chama amejitokeza kuwania nafasi hiyo ili kusaidia chama kushinda kwani anajua vema siasa za nchi ya Tanzania na asingependa kusikia jimbo la Arusha ni la upinzani bali jimbo ni mali ya Ccm kama ilivyo sasa.


Amempongeza Rais Samia Hassan Suluhu kwa kuruhusu mikutano ya Vyama vya Siasa hivyo kutokana na uzoefu wake katika nafasi zake alizokuwa nazo awali anaamini akipata nafasi ya ujumbe wa Halmshauri kuu atasaidia Chama.



“Ninauzoefu wa kisiasa na naomba ridhaa ya kuwania nafasi hii kwani sifa na uzoefu wa pande zote mbili katika chama ninao”

 

Milya ni Miongoni mwa vijana machachari wenye historia kubwa sana katika siasa na uongozi Mkoania Arusha na sasa anajaribu kuomba nafasi ya kugombea ujumbe wa NEC .

No comments: