WANUFAIKA TASAF WAHUSISHWE MIKOPO ASILIMIA 10 - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 13 July 2023

WANUFAIKA TASAF WAHUSISHWE MIKOPO ASILIMIA 10

 


NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete





NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete akiangalia Moja ya manufaa ya mradi wa Tasaf


NA JULIETH MKIRERI, MAIPAC KIBAHA 


maipacarusha20@gmail.com 

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete  ametoa maelekezo kwa Wakurugenzi wa Wilaya ya Kibaha kuwahusisha wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwenye mikopo ya asilimia kumi.

Kikwete ametoa maelekezo hayo juzi alipokuwa katika ziara yake ya kikazi kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha na Kibaha mjini mkoa wa Pwani.

Amesema wakurugenzi hao wanatakiwa kufikisha miradi ya asilimia kumi kwa walengwa wa wa TASAF ili nao waendelee kuboresha miradi waliyoanzisha kupitia mpango uanotekelezwa kwa kaya masikini.

Aidha amesema Serikali itaendelea kuwatafuta wananchi kutoka kaya masikini na kuwaingiza kwenye mpango wa TASAF ili waweze kunufaika na kuondoka kwenye hali duni walizonazo.

"Ndani ya Sera za Chama tawala cha Mapinduzi (CCM) maendeleo ya wananchi kwanza na Serikali haiwezi kukubali kuona wapo wananchi ambao  bado wanaishi kwenye hali ya umasikini ndio maana TASAF ipo kwa ajili ya kumaliza hali hiyo" amesema.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Kibaha Butamo Ndalahwa alisema ipo miradi ambayo inaendelea kutekelezwa na imekuwa na matokeo chanya kwa kubadilisha maisha ya walengwa ukilinganisha na hali zao kabla ya miradi kuanza.

Mratibu wa TASAF Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Sijaona Muhunzi alisema kitongoji Cha Mwembebaraza kata ya Janga ni miongoni mwa maeneo/Vijiji 46 vinavyotekeleza mpango wa kunusuru kaya maskini katika Halmashauri ya wilaya ya Kibaha.

Ameeleza kwamba kitongoji hicho kina Jumla ya kaya za walengwa 45 kati hizo  44 sawa na asilimia 98 zinalipwa kupitia mtandao ikiwemo simu na benki.

Muhunzi ameafanua, kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kitongoji kimepokea million 10,464,606 kwa ajili ya malipo ya walengwa ambapo kati ya fedha hizo 1,462,135 zinalipwa taslimu 9,002,471 zimelipwa kwa njia ya mtandao.

Amesema, katika kutekeleza mpango wa akiba na kukuza uchumi wa kaya wanalenga kuwajengea uwezo walengwa wa mpango kuweka akiba ndogo ndogo.

No comments: