Na: Mwandishi wetu
MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Erasto Makala amesema Madiwani na Watumishi wako kwa ajili ya kuwatumikia wananchi hivyo ni vema wakafanya kazi kwa bidii kutafuta kero zinazokwamisha maendeleo.
Makala amesema kwa pamoja wanatakiwa kuwahudumia wananchi kupitia mapato sambamba na kufanya mikutano kusikiliza kero na kuzitafutia ufumbuzi wa haraka..
Mwenyekiti huyo alitoa maelekezo hayo alipokuwa akizungumza kwenye Baraza lMaalumu la Madiwani lililoketi kupitisha Makisio ya Mpango wa Bajeti wa mwaka 2024/2025.
Katika kikao hicho Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha wamepitisha makisio ya mpango wa bajeti ya mwaka 2024/2025 sh. Biln 34.9 ambazo zinatarajiwa kukusanywa na kutumika kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Akisoma taarifa ya Makisio ya bajeti hiyo alibainisha kwamba kati ya fedha hizo sh. Biln 2.5 ni makusanyo ya ndani vyanzo visivyo na masharti, sh. Biln 1.5 makusanyo yatokanayo na Mfuko wa Afya wa Jamii, ada, Bima, malipo ya papo kwa papo, ada ya taka ngumu na duka la dawa, sh.19.7 ni Mishahara ya Watumishi, sh. Biln.1.5 ni matumizi ya kawaida na sh. Biln 10.3 ni miradi ya maendeleo.
Aidha alisema kati ya fedha hizo zaidi ya sh.Biln moja ni kupitia fedha za mapato ya ndani, sh. Biln 5.9 ni fedha za miradi za ndani (Serikali kuu) na sh. 3.3 fedha za wahisani).
Kadhalika alisema ,Mpango huo wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/2025 umeandaliwa kwa kuzingatia Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa miaka mitano awamu ya pili unaolenga Uchumi wa Viwanda, Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa 2020, Sheria ya Bajeti sura 439 na kanuni zake na Masuala yaliyosisitizwa katika mwongozo wa Mpango na Bajeti ya mwaka 2024/2025.
Amesema muongozo huo ni pamoja na kutenga asilimia 40 ya mapato ya nadani kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya kuwezesha vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.
Aisha, Fedha nyingine zitakazotengwa ni kwa ajili ya Lishe, shughuli za ustawi wa jamii, kuwezesha Watendaji wa Kata, ukamilishaji wa miradi viporo na miradi yakuongeza mapato ya Halmashauri kupitia fedha za mapato.
Makala amesema katika kipindi Cha mwaka wa fedha 2023/2024 Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha ilikadiria kukusanya jumla ya sh.. 33,520,944,664.00 kutoka katika vyanzo mbalimbali vya Halmashauri, na hadi kufikia Disemba 31, 2023 sh. Biln 16.8 zimekusanywa sawa na asilimia 50 ya makisio ya mwaka.
Amesema Mafanikio uwajibikaji na ushirikiano mzuri uliopo baina ya Watumishi na Uongozi wa Halmashauri kufanya ziara shirikishi za ufuatiliaji na utekelezaji wa maazimio yamewezesha kukusanya vizuri mapato ya Halmashauri hiyo.
Awali Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Edward Masona alisema watahakikiaha wanaimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kutenga fedha na kupeleka kwenye miradi ya maendeleo..
Masona amesema bajeti hiyo imezingatia dira ya Maendeleo ya Taifa, ilani ya Uchaguzi Mkuu na masuala yaliyosusitizwa katika muongozo wa mpango wa bajeti.
No comments:
Post a Comment