SIMANZI EDWARD NGOYAI LOWASSA AFARIKI DUNIA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday 10 February 2024

SIMANZI EDWARD NGOYAI LOWASSA AFARIKI DUNIA





Na: Mwandishi wetu, Arusha


maipacarusha20@gmail.com


Waziri Mkuu mstaafu wa  Tanzania,  Edward Ngoyai Lowassa amefariki dunia katika hospital ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, jijini Daresalaam alipokuwa anapatiwa matibabu.


Edward Lowassa alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania kwa kipindi cha mwaka 2005 hadi 2008 na kuweka rekodi ya kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanzania kujiuzulu wadhifa wake.


Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango akiwa Longido Mkoani Arusha ameutangazia umma kifo cha Waziri Mkuu Edward Lowasa kupitia Televisheni ya Taifa TBC 1. 


Amesema kufuatia kifo hicho RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluh Hassan ametangaza siku Tano za maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti.


"Ndugu watanzania wenzangu Rais Samia Suluhu anatangaza kifo cha Waziri Mkuu mstaafu  ambaye amefariki Leo saa nane mchana"amesema.


Amesema Lowassa amefariki akiwa anapatiwa matibabu JKCI kutokana na Ugonjwa kujikunja utumbo na matizo la mapafu 


Amesema awali Lowassa alikuwa amepelekwa kwa matibabu nchini Afrika Kusini akitoka JKCI  na baadaye  alirejea tena hospital ya JKCI Hadi Leo alipofariki.






No comments: