Na Queen Lema,Arusha
maipacarusha20@gmail.com
Mgahawa Wa Chefs Pride Dodoma umefanikiwa kutwaa tuzo ya mgahawa Bora wa chakula cha asili kwenye tuzo za Serengeti Awards zilizofanyika Arusha wiki iliyopita.
Akizumgumza Mara baada ya kutwaa tuzo hizo mkurugenzi mkuu wa Chefs Pride Bw Abubakar Bamiri Alisema kuwa wao kama wadau wa utalii wamefarijika Sana baada ya kupata tuzo hiyo.
Aliendelea kudai kuwa Mpaka wanapata tuzo hiyo ni heshima kubwa sana na wataendelea kufanya kazi kwa bidii Sana
Alifafanua kuwa wataendelea kuboresha huduma zao ili kuwavutia hata mataifa ya nje ambayo yanakuja kwenye shuguli mbalimbali za utalii
"Pamoja na yote tunaishukuru sana Serikali kuweza kuratibu tuzo hizo ambazo zinasabisha chachu ya uwajibikaji iwe kubwa na kuweza kutangaza nchi ya Tanzania"aliongeza.
Wakati huo huo aliwataka watanzania kuhakikisha kuwa wanautumia mgahawa Wa Chef's Pride Dodoma pamoja na Dar es salam kwa kuwa wamejipanga vyema kuanzia sasa na hata kwenye ugeni mkubwa wa kimataifa.
Tuzo hiyo ilikuwa miongoni mwa tuzo 51 zilizotolewa katika hafla kubwa iliyofanyika wiki iliopita katika Hoteli ya Mount Meru, jijini Arusha.
Naye Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, ambaye aliipongeza sekta ya utalii kwa mchango wake mkubwa katika kukuza uchumi wa taifa, kuongeza ajira, pamoja na kuitangaza Tanzania kimataifa kama kivutio bora cha utalii.
Alisisitiza kuwa ushirikiano kati ya serikali na wadau binafsi umeendelea kuleta matokeo chanya, hasa katika kuboresha miundombinu na huduma zinazowawezesha watalii kupata uzoefu bora wanapotembelea vivutio vya nchi
Mwisho

No comments:
Post a Comment