![]() |
| Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Rukia Zuberi akiwa ameambatana na Kamati ya usalama ya Wilaya hiyo, kukagua majengo ya hospitali ya Wilaya hiyo. |
Na Mwandishi Wetu, Mwanga
maipacarusha20@gmail.com
Mwanga: Mkuu wa Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, Rukia Zuberi, ametembelea Hospitali ya Wilaya ya Mwanga ili kujionea maendeleo ya shughuli mbalimbali za ujenzi zinazoendelea katika hospitali hiyo.
Mkuu huyo amesema kukamilika kwa ujenzi wa hospitali hiyo kutapunguza kwa kiasi kikubwa adha iliyokuwa ikiwakabili wananchi wa wilaya hiyo, ambao walilazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya.
Awali, wananchi wa Wilaya ya Mwanga walikuwa wakilazimika kwenda katika hospitali za rufaa na kibingwa zilizopo nje ya wilaya hiyo ili kupata huduma za afya, hali iliyosababisha usumbufu na gharama kubwa kwao.
Pamoja na mambo mengine ametembelea chuo cha ufundi Veta, kinachojengwa katika Wilaya hiyo, ambapo amesema kukamilika kwake kutasaidia kuwapatia vijana juzi mbalimbali zitakazowasaidia kujikwamua kiuchumi.



No comments:
Post a Comment