![]() |
| Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Rukia Zuberi akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 49 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi CCM |
![]() |
| Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Rukia Zuberi akiwa na mlezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro,Rabia Abdallah Hamidu katika maadhimisho ya miaka 49 ya chama cha Mapinduzi (CCM) |
Na mwandiahi wetu
maipacarusha20@gmail.com
Mwanga.Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Mkoani Kilimanjaro amewashukuru viongozi wa chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuonyesha ushirikiano wake baina yake na serikali akisema Wilaya hiyo ipo shwari na imetulia na wananachi wanaendelea na shughuli zao za kimaendeleo kama kawaida.
Mkuu huyo wa Wilaya, amesema ni heshima kubwa kwa Wanamwanga na kwamba ushirikiano huo umeonyesha wazi kuwa Wanamwanga wanakipenda chama hicho.
DC Rukia, aliyasema hayo Februari 3, 2026 wakati wa maadhimisho ya miaka 49 ya chama cha Mapinduzi (CCM)yaliuofanyika wilayani humo na kuhudhuriwa na wanachama, viongozi pamoja na wananchi mbalimbali kutoka katika Wilaya hiyo.
Katika maadhimisho hayo Mgeni rasmi alikuwa Mhe. Rabia Abdallah Hamidu, mlezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro, ambaye aliwahimiza wanachama kuendelea kushikamana, kudumisha mshikamano na kuenzi misingi ya chama tangu kuanzishwa kwake.
Mwisho.


No comments:
Post a Comment