NYUKI WAWAVAMIA WANAFUNZI 11 NA WALIMU WATATU LUKOBE MOROGORO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday, 13 February 2026

NYUKI WAWAVAMIA WANAFUNZI 11 NA WALIMU WATATU LUKOBE MOROGORO

 



Na Lilian Kasenene,Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


WANAFUNZI 11 na walimu watatu wa shule ya msingi kambi tano iliyopo mtaa wa kambi tano kata ya Lukobe Manispaa ya Morogoro wamevamiwa na nyuki na  kuwang'atwa 


Baada ya tukio hilo wamefikishwa katika kituo cha afya Lukobe na kupatiwa matibabu.


Nyuki hao waliwavamia wanafunzi wakati wakiendelea na masomo darasani ambapo mbali na kusababisha majeruhi hao lakini pia taharuki kwa wananchi wanayoishi jirani na shule hiyo kutokana na tukio hilo kuwa ni la pili kutokea kwenye mtaa huo huo.


Akitoa taarifa mara baada ya kumaliza kazi ya uokoaji kamanda wa kikosi cha zimamoto na uokoaji mkoa wa Morogoro Shabani Marugujo alisema walipokea taarifa ya tukio hilo kutoka Kwa polisi kata mkaguzi wa polisi Zuwena Mwita na walipofika shuleni hapo timu ya uokozi ikiongozwa na Stafu Sajenti Alexander Makuluni ilikuta kundi kubwa la nyuki likiwa limetanda angani.


Aliwataja waliong'atwa ni Agness Timbi, Mohamed Shabani,

Chiku Mussa, Hilari Athuman,

Sabri Mengi, Ismail Mohamed, Amani Msimbe, Jackob Mnyaki, Mustapha Hassan, Violeth Brutusu, Brightness Mlema, Neema Omary, Mswahibu Ibrahim na Rukia Seif.


"Nyuki walitanda juu ya anga lakini wengine walikuwa kwenye mnara uliokuwa umebeba tanki kubwa la maji ndipo tulipoamua kutumia kiwatirifu aina ya rungu kuwadhibiti nyuki hao na kuwaondoa wote na kuacha mazingira yakiwa salama," alisema Marugujo.


Aidha kamanda Marugujo alisema timu hiyo ya waokozi pia iliwachukua majeruhi na kuwapeleka kituo cha afya Cha kata ya Lukobe kwa matibabu zaidi.


Akisimulia tukio hilo mwenyekiti wa mtaa wa kambi tano Elianini Kimaro alisema tukio hilo la nyuki ni la pili kutokea kwenye mtaa huo ambapo tukio la kwanza likitokea mwaka jana na kusababisha kifo cha mtoto mmoja baada ya nyuki kuvamia makazi ya watu.


"Hawa nyuki waliovamia Leo pale shule walikuwa wallmeweka makazi kwenye tenkinla maji na hakuna aliyekuwa akijua kama Kuna nyuki katika eneo hilo hivyo watoto wakati wanacheza ghafla walitimka na kuwashambulia wanafunzi pamoja na walimu, amesema Kimaro.


Alisema katika tukio hilo mwalimu mmoja kati ya watatu ndio alionekana kuwa na hali mbaya baada ya kung'atwa na nyuki hao hata hivyo wote walitibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani.


Kuhusu ratiba za masomo Kimaro amesema baada ya tukio hilo wanafunzi wengi walikimbia na kurudi nyumbani huku wachache walikuwa wamefungiwa kwenye chumba vya madarasa hata hivyo baada ya hali kukaa sawa nao waliruhisiwa kurudi nyumbani na kwamba ratiba ya masomo itaendelea kesho kama kawaida.


Kwa upande wake diwani wa kata ya Lukobe Selestin Mbilinyi alisema baada ya nyuki hao kudhibitiwa na kikosi cha zimamoto na uokoaji sasa hali imetulia na kesho masomo yataendelea kama kawaida.


Baada ya tukio hili taharuki ilitanda kwa wazazi na walezi wa watoto wanaosoma kwenye shule ya kambitano na shule jingine ya jirani ya Lukobe, hata hivyo niliwaeleza wazazi kuwa hali ya usalama imerejea na kesho wawaruhusu watoto waende shule wakasome.


Mmoja wa wazazi wa watoto walionusurika kwenye tukio hilo Joseph Exavery ameuomba uongozi wa shule kujenga tabia ya kukagua mazingira ya shule hiyo mara Kwa mara Ili kubaini mapema kama Kuna makazi ya nyuki.


"Hii shule ipo nje ya mji kuna mazingira ambayo nyuki wanaweza kuweka makazi mfano maboma ya nyumba (mapagale), miti na mazao yanayovutia nyuki mfano alizeti na kipindi hiki jua Kali ndio nyuki wamekuwa wakijitokeza hivyo lazima walimu na viongozi wachukue tahadhari," alisema Exavery.


Mwisho.

No comments: