![]() |
| Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Denis Londo |
![]() |
| Mkurugenzi mkuu wa TBS Dk Ashura Katunzi |
Na Lilian Kasenene, Morogoro
maipacarusha20@gmail.com
SHIRIKA la Viwango Tanzania(TBS) limetakiwa kuhakikisha bidhaa na huduma zinazozalishwa na kuuzwa nchini zinakuwa zenye kukidhi viwango vya ubora, usalama na ushindani katika masoko ya ndani na ya kimataifa.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Denis Londo alieleza hayo katika uzinduzi wa Baraza la wafanyakazi la Shirika la viwango Tanzania TBS lililofanyika mjini Morogoro.
Londo alisema ili kutekeleza jukumu hilo kikamilifu,TBS inatakiwa kuweka mazingira bora ya kufanyia kazi, kuimarisha mshikamano miongoni mwa watumishi, kuimarisha uzingatiaji wa maadili, nidhamu na uwajibikaji.
"Kwa msingi huu, Baraza la Wafanyakazi linapaswa kuwa sehemu ya suluhisho katika kuimarisha tija, kuchochea ubunifu na kuongeza ufanisi wa Shirika, kwa kutoa ushauri wenye tija na kushirikiana kwa karibu na Menejimenti katika kutatua changamoto za kiutendaji pale zinapojitokeza,"alisema
Naibu Waziri Londo alitoa wito kwa Menejimenti na Wafanyakazi kuendelea kushirikiana kwa karibu, kutumia majukwaa rasmi kama Baraza katika kutatua changamoto kwa njia ya mazungumzo na maridhiano, na kuepuka misimamo isiyo na tija.
Alisema ni vyema Baraza likawa chombo chenye mchango chanya katika kuboresha mazingira ya kazi, kuimarisha ustawi wa wafanyakazi, na kuongeza ufanisi wa Shirika katika kutekeleza majukumu yake kisheria.
Aidha, alitumia uzinduzi huo kuikumbusha Menejimenti ya TBS kuwa Mabaraza ya Wafanyakazi si vyombo vya hiari bali ni matakwa ya kisheria hivyo, Menejimenti ina wajibu wa kutekeleza maamuzi yote yanayofikiwa katika Baraza.
Mabaraza ya Wafanyakazi kama vyombo muhimu vya kisheria vinavyolenga kuimarisha mahusiano mema kazini, kukuza majadiliano ya kijamii, na kuhakikisha haki na wajibu wa waajiri na wafanyakazi vinatekelezwa kwa uwiano na kwa maslahi mapana ya taasisi na Taifa.
Serikali inatarajia Mabaraza ya Wafanyakazi yawe majukwaa ya majadiliano ya hoja, kwa uwazi na kwa kuheshimiana badala ya kuwa vyanzo vya migogoro au misuguano isiyo na tija, akawataka wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi kuwa na jukumu kubwa na la heshima la Kuheshimu mipaka ya kisheria, kuwasilisha hoja kwa maslahi ya wafanyakazi wote, si ya mtu mmoja mmoja, kujenga mshikamano, kudumisha amani na nidhamu mahali kazi na kuweka tija ,ufanisi.
Mkurugenzi mkuu wa TBS Dk Ashura Katunzi akizungumza katika uzinduzi huo alisema Baraza hilo ni la 80 ambalo ni jipya na ni chombo muhimu katika sekta ya Viwanda na Biashara ambalo linaangalia majukumu ya taasisi na maslahi ya watumishi na kuzinduliwa kwake kunaongeza chachu ya kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi na tija.
Dk Katunzi alisema shirika litaendelea kuwahudumia watanzania na kuhakikisha linatimiza malengo na majukumu na kuchagiza kwa kuwezeaha sekta ya Viwanda na Biashara ili nchi ya Tanzania kufikia uchumi mkubwa ili kutekeleza maono ya serikali.
Aidha alisema kupitia mikakati iliyojiwekea ya miaka mitano ya 2026/2031 ambayo ni ku ndel a kupeleka huduma karibu kwa wananchi,kutela tija na kupunguza muda wa utoaji huduma.
Dk Katunzi pia alisema alisema taasisi imeweza kuongeza watumishi 105 ambao wameweza kupelekwa kwenye maeneo ya mipakani, ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya vitendea kazi na kuongeza ofisi za Kanda na matarajio wanatarajio kuongeza zaidi ofisi.
Mwisho.





No comments:
Post a Comment