MAONESHO YA MIFUGO KANDA YA ZIWA 2026, KUFANYIKA BUSANDA- SHINYANGA, WADAU WAKARIBISHWA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 24 March 2026

MAONESHO YA MIFUGO KANDA YA ZIWA 2026, KUFANYIKA BUSANDA- SHINYANGA, WADAU WAKARIBISHWA

 



Na. Mwandishi Wetu,


maipacarusha20@gmail.com 


MAONESHO ya Mifugo Kanda ya Ziwa (Lakezone Livestock Expo) yanatarajia kufanyika Mei 30-31 mwaka huu, Busanda Mkoani Shinyanga, ambapo wadau mbalimbali wa mifugo wanatarajiwa, kushiriki.


Kwa mujibu wa Diana Lukio Ambaye ni Mwandaaji wa maonesho hayo, amebainisha kuwa, yatawakutanisha wafugaji, wakulima na wadau wote kwenye mnyororo wa thamani kutoka Mikoa ya Shinyanga, Mara, Simiyu, Mwanza, Geita, Tabora na Kagera.


"Ni maonesho ya kihisitoria ambayo yatakuwa na vitu vingi vya kujifunza juu ya ufugaji wa kisasa, masoko, fedha, bima za mifugo, breeds and feeds za kisasa. 


"Karibu tujifunze na kuwekeza kwenye ufugaji biashara". Amesema Diana Lukio.


Aidha, kwa washiriki ama udhamini wanaweza kuwasilisha moja kwa moja na waandaji kwa namba +255762918153 


Ambapo kwa sasa hatua za awali zinaendelea za maonesho hayo.


Maonesho hayo ya mifugo Kanda ya Ziwa, ambapo yanaenda kwa kauli mbiu: "Ufugaji Biashara" pia yataambatana na mabanda mbalimbali ya wadau, huku kukiwa na shughuli za minada, maonesho, biashara ya bidhaa mbalimbali za mifugo na wadau na Ngoma za Asili.


Mwisho.

No comments: