Na mwandishi Wetu
maipacarusha20@gmail.com
Moshi: Mbunge wa Moshi Mjini (CCM), Ibrahim Shayo amewashukuru wananchi wa Jimbo hilo kwa kumwombea kufuatia ajali aliyopata Februari 18 mwaka huu akiwa kwenye ziara ya Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba akisema ajali hiyo ni mtihani wa Mwenyezi Mungu na kwamba haihusiani na mkono wa mtu.
Amesema chanzo cha ajali hiyo inatokana na tairi la mbele la gari walilokuwa wakisafiri kupasuka na dereva kushindwa kulimudu gari hilo ambalo lilikuwa katika spidi 160.
Mbunge huyo ameyasema hayo leo, Machi 8, alipokuwa akizungumza na wananachi wa jimbo hilo katika viwanja vya stendi ya mabasi mjini Moshi.
Mbunge huyo pia aliwashukuru wananachi kwa dua zao na kueleza kuwa sasa yupo tayari kuchapa kazi na kutekeleza ahadi zake za kampeni.
Shayo aliongeza kuwa anaamini ajali hiyo ilikuwa mtihani wa Mwenyezi Mungu, na anashukuru kuwa amepata nafuu na anaendelea na kazi kama kawaida .
Mwisho.



No comments:
Post a Comment