Rais Samia alivyoshiriki maadhimisho ya Siku ya Mashujaa Dodoma - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday, 25 July 2026

Rais Samia alivyoshiriki maadhimisho ya Siku ya Mashujaa Dodoma

 






Rais Samia Suluhu Hassan leo Julai 25, 2026, ameshiriki maadhimisho ya Kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, mkoani Dodoma.


Katika maadhimisho hayo, Rais Samia aliweka Silaha za Jadi na shada la maua kwenye Mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa kwa ajili ya kuwakumbuka mashujaa waliopigania na kulinda taifa.


Shughuli hiyo pia ilihusisha gwaride maalumu la maombolezo lililoandaliwa kwa heshima ya mashujaa wa taifa.

No comments: