Wananchi kutoka maeneo mbalimbali tayari wamewasili katika eneo la mradi wa umeme, kushuhudia leo Agosti 22, 2026, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiandika historia mpya ya kuzindua Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP) kinachozalisha umeme Megawati 2,115, kilichopo Rufiji mkoani Pwani.
Maelfu ya wananchi wameendelea kumiminika tayari kuwa sehemu ya kihistoria ya watakaoshuhudia uzinduzi wa mradi huu mkubwa wa kimkakati ambao umekuja kumaliza changamoto ya umeme nchini.
Mradi huu umetumia Sh. trilioni 7.452 kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya umeme ya uhakika itakayochochea maendeleo katika nyanja mbalimbali.


No comments:
Post a Comment