RC MAKALLA: UWEKAJI TAA UWANJA WA NDEGE ARUSHA UMEKAMILIKA,Amshukuru Mhe. Rais Samia kwa kutekeleza ahadi yake - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 26 August 2026

RC MAKALLA: UWEKAJI TAA UWANJA WA NDEGE ARUSHA UMEKAMILIKA,Amshukuru Mhe. Rais Samia kwa kutekeleza ahadi yake


 


Mkuu wa Mkoa Arusha CPA Amoss Makalla Asema kukamilika kwa uwekaji wa taa hizo kutarahisisha usafiri wa uhakika kwa abiria, kuchochea utalii na kufanikisha Bunge la IPU na AFCON





Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla ametangaza kukamilika kwa mradi wa uwekaji wa taa katika uwanja wa Ndege wa Arusha, akimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa ahadi yake hiyo aliyowaahidi wananchi wa Mkoa wa Arusha wakati wa Kampeni za uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.


Mhe. Makalla amebainisha hayo leo Jumanne Agosti 25, 2026 wakati wa ziara yake ya kukagua mradi huo, akisema kukamilika kwake kunafungua fursa zaidi ya kuchochea shughuli za utalii, biashara na uwekezaji pamoja na kurahisisha maandalizi ya Arusha kuwa mwenyeji wa Bunge la dunia IPU na AFCON 2027.


"Nimejiridhisha, nimewasha taa na nimeona zote zinawaka, Uwanja wetu upo salama na upo tayari kutumika na kukamilika kwa taa hizi ni sehemu ya maandalizi ya kufanikisha Bunge la dunia (IPU) mwezi Oktoba ambapo Wabunge kutoka Nchi mbalimbali watakuwa hapa na pia ni sehemu ya maandalizi ya michuano ya AFCON 2027 sasa washiriki watafika Mkoa wa Arusha moja kwa moja bila shida yoyote." Amesema Mhe. Makalla.


Kwa upande wake Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Arusha Bw. Edgar Mwankuga amemshukuru Mhe. Makalla kwa usimamizi wake wa karibu na msukumo wake wakati wote wa zoezi hilo la ufungaji wa taa uwanjani hapo, akibainisha kuwa kando ya kuchochea utalii na biashara Mkoani Arusha, uwanja huo kufanya kazi kwa saa 24 utasaidia pia kuongeza mapato ya Mkoa na serikali kwa ujumla.

No comments: