TEC : Tuliomba kikao na Rais Samia - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday, 14 August 2026

TEC : Tuliomba kikao na Rais Samia

 






Mwandishi Wetu maipac 


maipacarusha20@gmail.com 


Siku chache baada ya Rais Samia Suluhu Hassan, kuonana na viongozi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ( TEC), taasisi hiyo imefunguka ikieleza ndio iliyoomba kikao hicho, ili kujadili masuala mbalimbali yanayolenga kuliponya Taifa.


Hayo yamebainishwa Agosti 13,2026 na na Katibu Mkuu wa TEC, Padri Charles Kitima, kupitia picha jongefu iliyosambazwa kwa umma, kuhusu walichoteta kati yao na Rais Samia Agosti 10,2026 jijini Dodoma.


" Tuweke bayana kuwa hili kutano kati ya Maaskofu Katoliki Tanzania na Rais( Samia) lilikuwa ombi la maaskofu Katoliki, hawakuitwa bali waliomba kumuona Rais. Mwaka 2025, kabla ya uchaguzi mkuu maaskofu walimuomba Rais lakini hawakufanikiwa," amesema Padri Kitima. 


Ameongeza kuwa, "Kwa kuzingatia yaliyotokea kwenye uchaguzi mkuu,  na hali halisi ya kisiasa, mwaka huu maaskofu wakamuomba tena Rais  ili kumshirikisha mtazamo wao kuhusu hali iliyopo nchini," alisema Padri Kitima.


Padri Kitima amefafanua kuwa maaskofu wameweka bayana kuwa ili Taifa litoke hapa lilipo inapaswa kusimamia ukweli, kusameheana, kuridhiana na  kuponya nchi.

No comments: