Baadhi ya Wabunge wa Tanzania wakishiriki Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), wakijumuika na wabunge kutoka mataifa mbalimbali duniani kujadili masuala yanayohusu amani, usalama na maendeleo.
Katika mkutano huo, Kamati ya Kudumu ya Amani na Usalama wa Kimataifa ya IPU imejadili wajibu wa Mabunge katika kuhakikisha amani na usalama katika zama za matumizi ya Akili Unde (AI).
Mjadala huo umeangazia pia umuhimu wa demokrasia ya Kibunge, usuluhishi na mazungumzo katika kujenga mustakabali wa amani endelevu, pamoja na namna Mabunge yanavyoweza kutumia nafasi yao katika kuimarisha amani na usalama katika jamii na duniani.
#IPU153Tanzania

No comments:
Post a Comment