TANAPA YAFUTURISHA WATU WENYE UHITAJI PAMOJA NA KITUO CHA WATOTO YATIMA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday, 29 March 2025

TANAPA YAFUTURISHA WATU WENYE UHITAJI PAMOJA NA KITUO CHA WATOTO YATIMA









Na: Mwandishi Wetu, Maipac 


maipacarusha20@gmail.com 


Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzani limefanya zoezi la kufuturisha watu mbalimbali wenye uhitaji ambapo ni pamoja na Kituo cha Watoto yatima cha Al furqan welfare trust kilichopo mkoani Arusha, hafla ya Iftaar hiyo illifanyika katika ofisi za Makao Makuu ya Shirika Jijini Arusha leo Machi 27, 2025. 


Zoezi hilo ambalo linaonyesha matendo ya sala na huruma kwenye jamii lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini ya kiislamu wakiongozwa na Hussein mwijunje, Shekhe wa Wilaya ya Arusha, Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, Juma Mussa Kuji pamoja na watumishi wa TANAPA.


Katika Hafla hiyo iliyoambatana na sala, chakula cha usiku pia ilihusisha utoaji wa zawadi ambazo ni vyakula kwa kituo cha watoto yatima cha cha Al furqan welfare trust, zawadi hizo ni pamoja na vyakula, mafuta, katoni za maji, Soda pamoja na mbuzi mmoja.

No comments: