Washiriki kongamano la Ramadhani Qarim.uta - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 31 March 2025

Washiriki kongamano la Ramadhani Qarim.uta







Na: Burhani Yakub,Tanga.


maipacarusha20@gmail.com


Vijana wa kiislamu nchini wamehimizwa kusoma ipasavyo masomo ya uchumi,ufundi,afya na sayansi ili wawe wabobezi na msaada kwa jamii.


Diwani wa kata ya Central Jijini Tanga,Said Mbarouk ametoa wito huo jana wakati wa kongamano la vijana waislamu wa Mkoa wa Tanga (Ramadhani Qarim 2025) lililofanyika katika shule ya Sekondari ya Old Tanga jijini hapa.


Amesema vijana wa kiislamu watakapobobea katika masomo ya uchumi ufundi afya na sayansi wataweza kuisaidia jamii kwa sababu kutokana na kuijua dini yao kuna baadhi ya maeneo watalazimika kujitolea kwa hali na Mali.


"Ninahimiza mjikite katika ubobezi wa masuala hayo kwa sababu mnafahamu nini maana ya kuisaidia jamii na mnafahamu kuna malipo akhera"amesema Mbarouk.


Kwa suala zima la kuporomoka maadili, Mbarouk ambaye alimwakilisha Meya wa Halmashauri ya Jiji la Tanga amewataka wanawake kuwa walezi muhimu wa vijana kwa kuikemea mienendo mibaya majumbani.


"Kuporomoka kwa maadili kunaanzia majumbani kama wanawake mnawaachia wanenu kunaa mavazi yasiyofaa na kufanya wanavyotaka bila kuwakemea na kuwapa miongozo ya kidini basi mtambue kwamba huko tuendako hali itazidi kuwa mbaya zaidi"amesema Mbarouk.


Mratibu wa kongamano Hilo,Selemani Msey amesema lilianzishwa tangu mwaka 2018 lengo likiwa kuwakutanisha waislamu na vijana kwa ujumla katika mwezi wa Ramadhani na kutoa fursa kwa wabobezi wa dini na masuala ya kijamii ambao wamekuwa wakitoa mada mbalimbali.


"Mfano mwaka juzi tulifanya maandamano makubwa ya kupiga vita ushoga nchini kwetu,vivyo hivyo kila mwaka tumekuwa tukija na mada kulingana na mahitaji ya wakati huo,lengo ni kwanza kuwakutanisha waislamu pamoja na kujadili masuala mbalimbali na ifikapo magharibi tunafuturu kwa pamoja"amesema Msey.


Katika kongamano hilo,Diwani huyo pia alikabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi wasichana na wavulana wa shindano la kusoma Quran .


MWISHO

No comments: