Na Epifania Magingo,Manyara
maipacarusha20@gmail.com
Taasisi ya haki Elimu inayoshughulikia masuala ya Elimu hapa Nchini imefanya tafiti katika Upande wa Afya,lishe, Ulinzi na usalama wa mtoto anapokua katika mazingira ya shule na kubaini changamoto kadhaa ikiwemo usalama wa vyoo vinavyotumiwa na wanafunzi mashuleni ni mdogo.
Inaelezwa kuwa utafiti huo umelenga kupata maendeleo endelevu kuanzia ngazi ya Chini ya ukuaji wa mtoto katika maeneo hayo muhimu na kusisitizwa kuwa ili kuondoa udumavu katika nyanja zote yapaswa ukuaji ungaliwe tangu kipindi Cha ujauzito.
Hayo yamebainishwa katika ripoti iliyosomwa na Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara Benjamin Richard kwenye kikao Cha uwasilishaji wa ripoti ya ufuatiliaji wa uwajibikaji wa Jamii katika malezi na makuzi ya awali ya mtoto ambacho kimefanyika ukumbi wa White Rose Babati mjini.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa katika Upande wa lishe, shule nyingi zimekua zikijitahidi kutoa huduma ya chakula mashuleni na kwamba usalama wa uhifadhi wa chakula hicho umekua mdogo kwa baadhi ya shule na kuzua hofu ya kuvamiwa na sumu kuvu.
"Ili kuepusha sumu kuvu vyakula vitunzwe katika mazingira Salama,hata vyakula anavokula sio mchanganyiko kwaio tulitoa rai kwamba tunapotoa bajeti zetu basi tuweke mchanganyiko wa vyakula isiwe aina moja tu,manake watoto wataendelea kudumaa,tusipowajenga kiafya wataendelea kudumaa Zaidi".amesema Richard
Aisha, amesema suala la unyonyeshaji limekua changamoto kwa wamama wengi wananyonyesha chini ya mwaka 1 Hadi miezi 6 na kutozigatia taratibu za Afya Kutokana na uelewa mdogo.
Alizungumzia suala la Afya mashuleni Richard amesema usalama wa vyoo umekua sio salama kwakua wanafunzi wa awali wamekua wakitumia vyoo hivyo pamoja na wanafunzi wa umri mkubwa ambapo kati ya shule 16 zilizofanyiwa utafiti shule 5 tu zinavyoo vya wanafunzi wa awali.
"Vyoo salama bado ni changamoto kwaio tunapojenga vyoo tuhakikishe usalama Kwa kiwango kikubwa ili kuhakikisha watoto wetu wanakua na Afya ilionjema zaid". amesema Richard
Suala la ulinzi na usalama Kwa watoto hao imebainishwa kuwa asilimia kubwa ya wazazi waliohojiwa wamesema shule ziko salama na wanalindwa kwa usalama unaotakiwa kwakua shule zimetengeneza mifumo thabiti ya kupokea taarifa za kiusalama na kufanyiwa kazi.
"Changamoto ni kwamba shule hazina uzio,japokua usalama wa kuwalinda upo na shule nyingine zipo katibu na barabara,kwaio tuangalie katika bajeti zinazopangwa basi kuwekwe fensi".
Aidha,baadhi ya waliohojiwa walithibitisha kuwa adhabu za kuumiza mashuleni zimepungua kwa kiwango kikubwa hii itasaidia kupunguza vitendo vya kikatili na kusababisha mtoto kutopenda elimu hii pia inangaliwe na hata kwa mzazi kutompa adhabu Kali anapokua nyumbani.
Taarifa hiyo imebainisha kuwa suala la malezi ya watoto yazingatie mila na desturi zilizokua njema na hata katika dini zetu na kwamba jamii iwajibike moja kwa moja katika hilo.
Mganga Mfawidhi Hospital ya mji Babati Mkoa wa Manyara lupembe Francis amesema wazazi wanapaswa kutumia nguvu nyingi kipindi Cha ujauzito hasa katika miezi 3 ya mwanzo kwa kuzingatia lishe na kumjenga mtoto akue vizuri ili aondokane na udumavu ikiwemo wa akili jambo ambalo litakuja kuleta athari hapo baadae.
" Kipindi Cha miezi 3 ya mwanzo wenza wote wawili wanapaswa kwenda vituo vya Afya kupata elimu bora ya kumuandaa huyo mtoto kua bora hasa katika suala la akili,kwaio kama mtakua mmejiandaa vizuri katika malezi tangu awali inakua ni Bora zaidi".
Naye, Mwakilishi kutoka Haki Elimu Tanzania Pius Makomelelo amesema mapendekezo yote yaliyopendekezwa kwenye mtaala wa Elimu yatafanyiwa kazi na huku akidai kuwa hasa katika mtaala mpya wa Elimu ambayo tayari umezinduliwa rasmi na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia.
Amesema mapendekezo yaliyotelewa ni pamoja na kuboresha lishe kwenye shule za awali na msingi,kutilia mkazo Elimu ya Afya kwa wazazi na walezi na mengine mengi.
Takwimu za ripoti hiyo zimefanyika Mkoani Manyara kupitia katika kata 4 za babati ,bagara ,maisaka na nangara kwenye shule za msingi 16 ambapo wadau mbalimbali walihojiwa wakiwemo watendaji wa kata ,wamiliki wa vituo vya kulelea watoto day care ,walimu ,viongozi wa serikali za mitaa na vijiji ,wawakilishi wa asasi za kiraia pamoja na wazazi wenye watoto katika shule za awali.
Hata hivyo kuhusu adhabu kwa watoto tafiti zimeonesha asilimia 11.2 ya waliohojiwa wamethibitisha kuwepo kwa adhabu za kuumiza kwenye baadhi ya shule.
Kwa upande wa malezi na muda wa wazazi kukaa na watoto asilimia 93.7 ya watu 168 walihojiwa na walikiri kuwa wazazi wengi hawana muda wa kukaa au kucheza na watoto wao.
Kwani wazazi wengi wamekua wakiacha majukumu yao kwa wasaidizi wa kazi za ndani,ambao mara nyingi huonekana kama mama na baba wa watoto hao.
Hivyo baada ya uwasilishaji wa ripoti hiyo Mwenyekiti wa kikosi kazi cha marafiki wa Elimu Babati Gaudensia Igoshalimo ,amesema kuwa watarejea kwa wananchi kwaajili ya kuhamasisha marekehisho ya changamoto zilizoonekana.
No comments:
Post a Comment