Na Lilian Kasenene, Morogoro
maipacarusha20@gmail.com
MABARAZA ya Watumiaji wa huduma mbalimbali yametakiwa kutoa elimu juu ya wajibu na haki kwa wateja wao.
Mwenyekiti wa jukwaa la Watumiaji Tanzania (TCF), Daudi Daudi amesema mabaraza hayo pia yanatakiwa kutoa elimu ya utunzaji wa taarifa za Watumiaji Ili zisiangukie kwa wahatifu.
Daudi ambaye ni Katibu Mtendaji wa LATRA-CCC amesema mabaraza ya Watumiaji yanawajibika kuwaelimisha wateja wao juu ya haki na msisha endelevu
Mwenyekiti huyo alisema kwa Watumiaji wa huduma za mawasiliano mabaraza yatoe elimu ya utunzaji wa taarifa zao binafsi Ili zisifikiwe na wahatifu.
Was,shiriki wa jukwaa hilo la kilele Cha wiki ya huduma za Watumiaji walisema asilimia kubwa ya wateja wao hawana uelewa wa ktosha juu ya wajibu na haki zao
Washiriki hao wamesema Watumiaji hawajui ni wapi wanaweza kupeleka malalamiko yao pale wanapotimiza wajibu wao lakini wakakosa huduma.
Samuel Msuya mshiriki wa jukwaa hilo alisema Kuna wakati changamoto zinasababishwa na Watumiaji wenyewe kwa kukosa uelewa au kuwa na tamaa.
"Watumiaji wanaotapeliwa mitandaoni ndio wanaosaidia kuibiwa kwa kutoa ushirikiano kwa matapeli kwa kuwapa taarifa zao". Aslisema Msuya
Mwenyekiti wa chama Cha albino mkoani Morogoro Hassan Mikazi alisema kamati za kupokea malalamiko ya Watumiaji hazijulikani hivyo kufanya wananchi wakose wapi pa kupeleka malalamiko yao wanapokosa huduma
Alisema wananchi wanatimiza wajibu wao kwa kulipia huduma lakini hawapayi haki ya huduma walizolipia na hawajui wapi wapeleke malalamiko yao
Mikazi alisema Ili kuwepo na haki kwa pande zote mbili ni muhimu kuwepo na mikataba kati ya mtoaji na mpokeaji huduma Ili Kila upande utimize wajibu wake.
...
No comments:
Post a Comment