UHIFADHI ULIVYOWANUFAISHA WAKAZI WA KIJIJI CHA SANGAIWE - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday, 15 March 2025

UHIFADHI ULIVYOWANUFAISHA WAKAZI WA KIJIJI CHA SANGAIWE

 





Na Epifania Magingo, Manyara 


maipacarusha20@gmail.com 


Waswahili wanasema "baada ya dhiki farajà",msemo huu unajidhihirisha kwenye Kijiji Cha Sangaiwe kilichopo Kata ya Mwada Babati Vijijini Mkoa wa Manyara baada ya wananchi kuchukua jukumu la kutoa maeneo yao ya ardhi kwa Serikali ya Kijiji ili kufanya uhifadhi wa wanyama pori pamoja na Uwekezaji ambao unaleta tija kwa Jamii na Taifa kwa ujumla.


Historia ya uhifadhi inayofanyika katika Kijiji Cha Sangaiwe inaelezwa kuwa changamoto ya uharibifu wa mazao kutoka kwa wanyama pori iligeuzwa kuwa fursa na kwamba Sangaiwe ni miongoni mwa vijiji vitano ambavyo viliunda Jumuiya ya Wanyama Pori Burunge ambapo Kwa Sasa vipo Vijiji kumi hii ni Kutokana na baada ya wananchi kupata Elimu ya kutosha kuhusu uhifadhi na kuruhuhu Uwekezaji ambao ulianza kufanyika tangu mwaka 2013.


Mwenyekiti wa Kijijini Cha Sangaiwe Marian Mbere ameeleza mafanikio makubwa yanayopatikana ndani ya Kijiji hicho kutokana na uhifadhi ikiwemo kujenga Zahanati ya kisasa,Ofisi ya Kijiji, shule mbili za Msingi,kutoa chakula kwa wanafunzi,kuchangia ada kwa wanafunzi wanaojiunga na kidato Cha Tano na vyuo vikuu Kwa Kaya duni pamoja na mengine mengi. 


"Matokeo Chanya tunayaona Moja kwa moja,tunawapeleka watoto shule hizi za kulipia tunawasapoti wagonjwa wanaopata matatizo makubwa makubwa na hata hivo ajira zinapatikana ndani ya hotel zetu Vijana wetu wamepata ajira ndani ya hoteli".amesema Marian 


Amesema Kijiji hicho kimekuwa kikusanya kiasi kikubwa Cha mapato yake Kutokana na uwepo wa vyanzo vingi vya mapato ikiwemo hotel zilizopo na kuleta chachu ya ukuaji kwa kasi wa maendeleo.


Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kijiji Cha Sangaiwe Latifa Maida ameeleza changamoto kubwa inayoikabili Zahanati hiyo ni uchakavu wa barabara zinazoifikia katika Zahanati hiyo kwakua inaleta changamoto hata katika utaoji huduma kwa wananchi waliopo mbali na eneo hilo.


" Zaidi kuna barabara inatoka kibao Cha tembo kufika hapa Zahanati,na kutoka hapa Zahanati kufika hospitali ya Wilaya,na kutoka kwenye kitongoji Cha osole na wananchi kutoka vitongoji vya juu kuja huku Zahanati na kwenyewe hakupiti kabisa,Sasa itaanza kupelekea wamama kuzalia majumbani maana akifikiria pilikipiki inakua ni changamoto". amesema Latifa 


Katika risala iliyosomwa na Kaimu Mtendaji wa Kijiji Cha Sangaiwe Joseph Hosea amesema kijiji hicho kilitenga eneo lake kwaajili ya uhifadhi ambapo Kwa Sasa kuna wawekezaji watano,ambapo kimekuwa na mafanikio makubwa kwa kujipatia fedha nyingi ambazo zinatumika katika miradi ya maendeleo.


"Kijiji Cha Sangaiwe ni mwanachama wa JUHIBU,na makusanyo ya mapato kutoka Jumuiya ya hifadhi ya Wanyama Pori Burunge na hoteli ndani ya Kijiji kuanzia mwaka 2020 hadi 2025 kwa asilimia 60 zilizotokana na Utalii kwa miaka hiyo mitano ni Shilingi bilioni 2 milioni 101 laki 5 na 35 elfu na 23 na senti  69".


Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara Emanuela Kaganda amewapongeza wanakijiji wa Sangaiwe Kwa jitihada hizo za kutenga maeneo kwaajili ya uhifadhi na kusema kuwa ukusanyaji wa mapato kwa mwaka 2021 hadi 2025 Kijiji kimekusanya zaidi ya bilioni 2.4 ambapo fedha hizo zimetumika katika miradi ya maendeleo.


"Zahanati mbalimbali zimejengwa na kijiji na sio kuishia kujenga tu wameweka vifaa vya maabara katika Zahanati na kufunga mifumo ya ukusanyaji wa fedha lakini pia wanaendelea kutoa msaada kwa wananchi nimeongea na Mwenyekiti pamoja na mganga Mfawidhi wa Zahanati hii wameshajadiliana na kuzungumza kwamba waweze kutoa bima za Afya kwa wanakijiji wote". amesema kaganda


Kaganda ameeleza jinsi ambavyo Kijiji hicho kinanufaika na uhifadhi huo pamoja na kununua chakula kwaajili ya watoto wa awali hadi Sekondari kwa eneo hilo na kuwasomesha wanafunzi wanaofaulu kujiunga na kidato Cha tano na hata wa vyuo vikuu Kwa kuchangia Shilingi laki Saba kwa Kila mmoja na Shilingi laki Tano kwa mwananchi ambae atapata changamoto za kiafya kwaajili ya matibabu zaidi.


Kiongozi huyo àmetoa rai kwa Vijiji vingine hapa Nchini vinavyopata changamoto ya Wanyama Pori kufika katika Kijiji Cha Sangaiwe kujifunza ili kupata ujuzi ambao utabadilisha changamoto ya Wanyama na kua fursa ya kimaendeleo.


"Badala ya kuuwa wale tembo tuwatuze tuwaone na sisi na wageni kutoka nje waje kuona na watuachie Dola na baada ya hapo tuweze kuimarisha Uchumi wetu". amesema Kaganda 


Mkuu wa Wilaya Kaganda ametoa ahadi kwa Kijiji Cha Sangaiwe kwamba Serikali itaendelea kuwaunga mkono na kuwatengenezea mazingira wezeshi ya Uwekezaji ili Kijiji hicho kiendelee kukua kiutalii na kiuchumi.


Sangaiwe ni Kijiji Cha kwanza katika vijiji vilivyopo Nchini Tanzania kufanya uhifadhi na Utalii huku ikielezwa changamoto ya uharibifu wa mazao yao kutoka kwa Wanyama Pori imekua fursa ya kupata maendeleo kwa kuamua kuacha shughuli za Kilimo na kufanya uhifadhi  na kuruhuhu Uwekezaji ambao unaleta  tija kwa Jamii na Taifa na ikitajwa kuwa kinapokea mgao wa asilimia 60 ya mapato na kuelekeza kwenye miradi ya maendeleo ndani ya Kijiji hicho.

No comments: