TUME YA HAKI ZA BINADAMU YAWANOA WAANDISHI WA HABARI MANYARA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 25 March 2025

TUME YA HAKI ZA BINADAMU YAWANOA WAANDISHI WA HABARI MANYARA





 Na Epifania Magingo,Manyara 


maipacarusha20@gmail.com 


Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imetoa mafunzo na kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari Mkoani Manyara kwa lengo la kuwawezesha kuelewa na kuandika kwa usahihi masuala ya haki za binadamu.


Tume hiyo ina jukumu la kuhamasisha haki za binadamu na utawala bora na kufanya uchunguzi mbalimbali zinazohusiana na ukwiukwaji wa misingi ya utawala bora na haki za binadamu,kutoa elimu kwa umma, kufanya tafiti pamoja na  kuishauri serikali kuhusu haki za binadamu.


Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Mohammed Hamadi amesema kwa kuzingatia majukumu hayo ya tume wameandaa ziara ya kutoa elimu kwa umma ,kwa kutembelea vituo vya polisi na magereza ,kufanya mikutano ya hazara kupitia watendaji wa kata katika wilaya, kutoa elimu kwa wanafunzi wa vyuo na shule mbalimbali.


"Tume tunakagua maeneo yote, tutatembelea pia magerezani ili tujue changamoto zao, kwa ujumla ziara yetu tutatembelea maeneo mengi tunataka wananchi wengi wapate uelewa". amesema Mohamed 


Aidha amesema  kuwa watu wakitambua haki zao, wataheshimu haki za binadamu na kusaidia kujenga jamii yenye usawa hivyo Mafunzo hayo yamefanyika katika jitihada za kuhakikisha wananchi wanatambua haki zao na kuhimiza uwajibikaji katika jamii.


Akizungumza katika mafunzo hayo, Halfan Rajab Botea, Ambae ni Afisa uchunguzi kutoka Tume ya Haki na Utawala Bora, amesema kuwa jamii ina wajibu wa kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa hususani kwa makundi maalumu kama walemavu, watoto na wazee,ili kuondokana na mila na desturi zilizopitwa na wakati ambazo zinachangia uvunjifu wa haki za binadamu. 


"Ukizingatia haki za binadamu lazima kutakua na utulivu na amani katika Jamii yetu,nchi yetu na Miata yetu,inakupa uhuru wa kufanya kazi na kuongeza Uchumi,ukizingatia haki hizo lazima vitendo vya kikatili vitapungua,wananchi wanapaswa kujua haki zao mfano kumiliki Mali kwa njia halali".


Nae, Monika Mnasha ambae ni Mkurugenzi wa Idara ya Elimu kwa UMMA ,mawasiliano na utafiti amesema watakuwepo Mkoani Manyara kuanzia 19 marchi hadi 28 march katika Halmashauri zote na Wilaya zote jambo kubwa ni kuwawezesha wananchi kufahamu haki za binadamu na utawala bora.



Katika ziara hiyo, tume pia itafanya mikutano ya hadhara ili kusikiliza malalamiko ya wananchi kuhusu haki zao pia watembelea shule mbalimbali kwaajili ya kutoa elimu huhusu haki za watoto, kufungua clubs za haki za binadamu pamoja na kufika kwenye vyombo vya habari kwaajili ya kutoa elimu.


" Sisi kama tume tumeamua kuanzisha Klabu za watoto mashuleni ili wajifunze na wao pia watatoa Elimu kwa watoto wengine kuhusu pia matendo ya uvunjifu wa haki za binadamu,tutatumia mbinu mbalimbali ili waweze kuelewa hata kwa kupitia nyimbo na ngonjera kwa Upande wa vyuo tunakua na mhadahalo".amesema Monika

No comments: