WATU WATATU WATEKETEA KWA MOTO MOROGORO NI BAADA YA LORI KUKONGANA USO NA KUTEKETEA KWA MOTO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 4 March 2025

WATU WATATU WATEKETEA KWA MOTO MOROGORO NI BAADA YA LORI KUKONGANA USO NA KUTEKETEA KWA MOTO

 








Na Lilian Kasenene, Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


WATU watatu majina hayajafahamika wamefariki Dunia kwa kuteketea na moto baada ya ajali ya magari mawili ya mizigo kugongana nayo kuteketea Kwa moto.


Tukio hiko limetokea usiku wa kuamkia Machi 4,2025 eneo la nanenane kata ya Tungi Barbara kuu ya Morogoro kwenda Dar  es salaam


Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Alex Mkama akizungumza na  waandishi wa habari alisema magari mawili yaligongana uso Kwa uso wakati yakipishana kwenye tuta la kupunguza mwendokasi.


Mkama alisema baada ya magari hayo kugongana yalishika moto na kuteketea na kusababisha vifo vya madereva wawili na abiria moja..


Kamanda huyo alisema, magari hayo moja wapo lilikuwa limebeba shehema ya mafuta aina ya Diesel katika Lori lenye namba za usajili RL6652 ya nchini Rwanda ambayo iligongana na gari namba T 374 DLC Scania Continental mali ya kampuni ya Reliable.


Alisema baada ya ajali hiyo kikosi Cha uokoaji Cha zimamoto na vyombo vingine vya usalama vilidhibiti moto huo ili usiendelee kuleta madhara zaidi.


Kamanda huyo alieleza uchunguzi wa awali katika eneo Hilo umebaini kuwa chanzo Cha tukio Hilo la ajali ni pale dereva wa gari lililotokea upande wa Morogoro kwenda Dar es salaam lililokuwa tupu hivyo kushindwa kudhibiti mwendo na gari lake na kusababisha kuhamia upande wa mwenzake aliyekuwa akitokea Dar es salaam ikiwa na shehema ya mafuta.


Alisema miili ya marehemu hapo watatu imehifadhiwa chumba ya kuhifadhi maiti hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro,ambapo alitoa wito Kwa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kupunguza mwendo maeneo yanayomtaka kufanya hivyo ili kuzika ajali zinazosababishwa na uzembe wa madereva .


Baadhi ya mashuhuda akiwemo Juma Ramadhani na Mkombozi Mwengele  walisema ajali kama hizo zinatakiwa kudhibitiwa na madereva wenyewe kwani baadhi Yao wao ndio wamekuwa chanzo Cha ajali nyingi nchini.

......


No comments: