Burhani Yakub, Tanga.
maipacarusha20@gmail.com
Watu milioni 2.2 waliopo katika mikoa 23 ya Tanzania Bara wamefikiwa na jopo la wataalamu wanaotoa msaada wa kisheria kupitia kampeni ya Mama Samia Legal Aid inayojumuisha wataalamu kutoka Wzara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na chama cha Wanasheria Tanganyika Law Society (TLS)
Taarifa hiyo imetolewa leo jioni na Afisa Uchunguzi Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria na Mratibu wa kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Mkoa wa Tanga,Laulent Burilo wakati wa mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Balozi Dkt Batilda Burian na waandishi wa habari wa kutangaza siku ya uzinduzi wa kampeni hiyo itakayofanyika katika Halmashauri 11 kuanzia Aprili 8 mwaka huu.
Amesema hadi sasa kampeni hiyo imeshafanyika katika mikoa 23 ambapo jumla ya watu milioni 2.2 wanefikiwa na kupokea migogoro 20,000 huku 4000 ikiwa imetatuliwa na kuisha kabisa.
"Katika mikoa 23 ambayo tumeshaendesha kampeni hii mashauri mengi na malalamiko yaliyoongoza ni migogoro ya ardhi ambayo takribani kila Halmashauri tuliyopita imejitokeza Kwa wingi"amesema Burilo.
Amesema Kwa Mkoa wa Tanga itaazinduliwa Aprili 8 na kufikia tamati Aprili 17 ambapo kila Halmashauri zitafikiwa kata 10 vijiji au mitaa mitatu ambapo mbali ya wanasheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria na Chama Cha Wanasheria wa TLS pia watakuwepo wataalamu kutoka dawati la jinsia la jeshi la Polisi,vizazi na vifo, kamishna wa ardhi,ofisi ya Mkuu wa Mkoa,idara ya ustawi wa jamii na maendeleo ya jamii.
Akizungumzia katika mkutano huo,Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Dr Buriani amewataka wanachi wenye changamoto mbalimbali kutumia fursa hiyo kujitokeza ili ziweze kitatuliwa.
"Hapa ni mahala muafaka,tumesikia mikoa ya wenzetu wengi wametatuliwa migogoro yao iloyodumu miaka mingi bila ufumbuzi...tujitokeze Kwa sababu wataalamu wote watakuwepo"amesema Dr Buriani.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema msaada huo utatolewa bure na kwamba wale ambao mashauri yao yatatakiwa kufikishwa mahakamani watapewa mawakili ambao gharama zote zitalipwa na Serikali Kwa muda wote ufumbuzi utakapopatikana.
MWISHO
No comments:
Post a Comment