WAMILIKI NA MAMENEJA KUMBI ZA STAREHE ARUSHA WAPATIWA ELIMU YA MADHARA YA DAWA ZA KULEVYA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 9 April 2025

WAMILIKI NA MAMENEJA KUMBI ZA STAREHE ARUSHA WAPATIWA ELIMU YA MADHARA YA DAWA ZA KULEVYA

 






Na Prisca Libaga Arusha


maipacarusha20@gmail.com 


Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 07.04.2025 jijini Arusha imetoa elimu kinga kwa wamiliki na wasimamizi wa kumbi na sehemu za sterehe na burudani wapatao 18 kuhusu madhara ya dawa za kulevya pamoja na kuwapatia mbinu wanazoweza kutumia katika udhibiti wa matumizi ya dawa za kulevya katika maeneo yao ya kazi wanayoyasimamia.


Aidha, Wasimamizi wa maeneo hayo ya starehe  walielezwa hatari na madhara ya kiafya ya kuchanganya Shisha na dawa za kulevya  kuwa adhabu yake ukibainika kutenda kosa hilo ni kifungo cha miaka mitatu na faini isiyopungua shilingi za kitanzania milioni tano au adhabu zote mbili kwa pamoja. 


Wamiliki na Mameneja wa Kumbi na maeneo ya Starehe walioshiriki Kikaokazi hicho waliombwa kuwa Mabalozi wa Mamlaka katika kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya katika maeneo yao ya kazi wanayoyasimamia ambapo katika kutilia mkazo suala hilo Ofisi ya Mamlaka Kanda ya Kaskazini iliandaa Mkataba rafiki kati ya Ofisi hii na Walimiki/Mameneja walioshiriki Kikaokazi hicho wa kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya katika maeneo hayo ya kazi.


Wadau walioshiriki Kikaokazi hicho wameishukuru Mamlaka kwa kuwapatiwa elimu ya madhara ya kujihusisha na dawa za kulevya na kuahidi kuwa Mabalozi wema wa Mamlaka na mwisho walikumbushwa wajibu wao wa kuendelea kushirikiana na Mamlaka kwa kutoa taarifa za wahalifu wa dawa za kulevya kwa kupiga simu ya bure 119.


MWISHO.

No comments: