SERIKALI YAJA NA CHANJO YA MAGONJWA YA MIDOMO NA KWATO KWA MIFUGO NCHINI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 9 April 2025

SERIKALI YAJA NA CHANJO YA MAGONJWA YA MIDOMO NA KWATO KWA MIFUGO NCHINI

 


Na Prisca Libaga Arusha


maipacarusha20@gmail.com 


Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha wafugaji Tanzania CCWT Taifa Kusundwa  Wamalwa amesema serikali kwa kushirikiana CCWT wameandaa mpango wa chanjo kwa mifugo hususani kwenye magonjwa ya kwato na midomo.


Aidha wafugaji nchini wametakiwa pindi zoezi la chanjo ya midomo na kwato litakapoanza kujitokeza kuwachanja mifugo yao kwa wakati uliopangwa na serikali ili kuepuka muda uliowekwa kupita kutokana na kuhamahama kufuata malisho sanjari na kuepuka faini zinazotozwa kwao.


Wamalwa akiongea jijini Arusha mapema Leo wakati wa ziara yao kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Missaile Mussa amesema lengo la ziara hiyo ni kujenga mahusiano na ukaribu kwa serikali yatakayosaidia kuwafikia wafugaji wote nchini hivyo kuongeza tija ya uzalishaji.


Amesema kwamba mifugo yetu lazima ichanjwe na kutambuliwa kwa kuweka alama za vipini ili  kupata cheti cha ubora kitakachowasaidia kufikia masoko ya kimataifa kwani baada ya mkutano wetu wa Uganda tumebani nchi kuwa tupo chini katika suala zima la chanjo ya midomo na kwato hivyo kushindwa kupata vyeti vya ubora.


Amesema suala la maeneo ya malisho ya mifugo lipewe kipaumbele katika suala zima la matumizi bora ya Ardhi nchi jambo litakalosaidia kuongeza ukaribu wa wafugaji na kuondoa njia ya kuhamahama kutafuta malisho hivyo kuongeza wigo wa utunzaji wa mazingira.


"Serikali imeweka fedha za ruzuku hasa vijijini katika suala zima la chanjo lakini kuna watendaji ambao wamekuwa hawawaaliki wafugaji ipasavyo kipindi hicho ili mwisho wawapige faini muda unapoisha hivyo tunawasihi wataalamu kuendelea kutoa elimu kwa umma ili jamii itimize wajibu wa chanjo"


Alisema Serikali ya jamhuri ya Muungano teyari imeshaandaa Chanjo itakayodumu kwa muda wa miaka 5 Chanjo hiyo itakapofanyika wafugaji wote wahakikishe wanatoa mifugo yao nawaifikishe kwenye chanjo ili kusaidia kuwa na ubora unaohitajika katika masoko ya kimataifa.


Awali Mjumbe wa kamati tendaji Taifa wa chama hicho Dkt. Christopher Nzella amesema serikali imefanya hamasa kubwa ya hili zoezi la chanjo ambalo litadumu kwa kipindi cha miaka 5 ambapo elimu hiyo inaendelea kutolewa kwenye mahali pote jinsi inavyotolewa.


Amesema serikali imefanya tafiti za kina katika zoezi zima la kuhakikisha chanjo inafanikiwa sanjari na kuacha kufuga kimazoea ikiwemo kutenga maeneo ya malisho katika mfumo mzima wa mayumizi sahihi ya ardhi.


Kwa Upande wake Rumay Bajuta Mwenyekiti kanda ya kaskazini CCWT Taifa amesema zoezi hilo Tangu mwaka 2023 serikali imekuwa ikihamasisha wafugaji wote nchi nzima hata kama ana eneo dogo wajitegemee kwa malisho kupitia mpango wa matumizi bora ya Ardhi.


Amesema kwamba tumeweka mkakati wa kutenga maeneo ya malisho kwa mpango wa matumizi bora ya Ardhi katika kila kijiji kwa mikoa yetu ya kanda ya kaskazini lakini kwa wilaya ya Mbulu tumetenge maeneo ya malisho 


"Ufugaji wetu kila mwaka au miaka miwili lazima kuvuna mifugo hususani madume na sio lazima tujikite kwenye ufugaji pekee tunaweza kuuza madume kujenga nyumba au kufanya biashara nyingine hii itasaidia kufuga kibiashara badala ya mazoea"


Mwisho.

No comments: