Na Lilian Kasenene,Kilombero
maipacarusha20@gamil.com
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dustan Kyobya amekipongeza Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali (TAGCO) kwa kutangaza utalii wa ndani baada ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa.
Kyobya aliyasema hayo mara baada ya maafisa hao wa serikali kutembelea hifadhi ya Taifa ya Udzungwa.
Alisema limekuwa jambo jema kwa maafisa hao wa serikali kufika katika hifadhi hiyo ya Taifa na kujionea vivutio vilivyopo katika hifadhi hiyo kwasababu wanayo nafasi kubwa ya kutangaza vivutio mbalimbali hapa nchini.
“Nimefarijika niliposikia kundi hili kubwa linafika katika wilaya yetu kubwa ya kimkakati kwa sababu ni wilaya inayozalisha umeme, sukari, na mpunga, pamoja na kusimamia uhifadhi,"alisema.
Hata hivyo alisema wilaya yake inaongoza kwa utalii kupitia hifadhi ya Taifa ya milima ya Udzungwa ambayo imezungukwa vivutio vingi ndani yake.
Mkuu huyo wa Wilaya Kyobya alisema Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia kutoa zaidi ya bililioni 4 kwaajili ya kujenga utalii wa kupita juu ya kamba katika maporomoko ya Sanje yaliyopo milima ya Udzungwa.
Naye, Mwenyekiti wa TAGCO Karimu Meshack alisema kwamba wametumia Mkutano Mkuu wa Mwaka kuwapatia mafunzo mbalimbali wajumbe hivyo wameona ni fursa pia ya kutembelea hifadhi hiyo kuunga mkono juhudu za Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutangaza vivutio vya utalii na kuhamasisha utalii wa ndani.
Aidha, Meshack aliahidi kutumia Jarida la Serikali Yetu linalomilikiwa na TAGCO kutangaza utalii wa milima na maporoko ya Udzungwa ikiwa ni sehemu ya mchango wa Chama kutangaza utalii wa ndani nchini na nje ya mipaka ya Tanzania.
Maafisa hao wamefanya utalii katika Hifadhi hiyo baada ya kufanya mkutano wao mkoani Morogoro.
......
No comments:
Post a Comment