WAFUGAJI WAHIMIZWA KUENDELEZA NA KUWEKEZA KIBIASHARA KWENYE SEKTA YA MIFUGO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 15 April 2025

WAFUGAJI WAHIMIZWA KUENDELEZA NA KUWEKEZA KIBIASHARA KWENYE SEKTA YA MIFUGO

 

KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Riziki Shemdoe 









Na Lilian Kasenene,Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Riziki Shemdoe amehimiza wafugaji nchini wakiwemo vijana kuanzisha, kumiliki, kuandaa maeneo, kuyaendeleza na kuyawekea miundombinu kwa ajili ya ufugaji ili kuwekeza kibiashara katika sekta ya mifugo.


Aidha amesema kuwa katika kuwekeza huko ni kukabiliana na changamoto ya ufugaji wa kuhamahama unaochangia migogoro ya ardhi.


Prof Shemdoe alisema hayo mkoani Morogoro kwenye siku ya Nyanda za Malisho Tanzania inayokwenda sambamba na kongamano la kisayansi la wataalamu wa sekta hiyo.


Alisema serikali kupitia Programu ya Jenga Kesho iliyo Bora(Build a Better Tomorrow)(BBT) imeweza kuwapatia ekari kumi(10) vijana 106 katika Ranchi ya Kagoma wakiwa vikundi 20 kwa kuwapatia mikopo kupitia banki ya Maendeleo ya Kilimo(TADB) ambapo walipatiwa jumla ya sh Mil 934,231,000.


Aidha katibu mkuu huyo alisema katika kukabiliana na changamoto za wafugaji kuhusu upatikanaji wa Malisho na maji kwenye Nyanda za Malisho Wizara kwa kushirikiana na wadau wa Mifugo inaendelea kuweka miundombinu ya maji katika maeneo mbalimbali nchini.


"Serikali pekee haiwezi kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya maji mabwawa na visima virefu kwa mara Moja, hivyo wafugaji wanahamasishwa kushiriki katika uchimbaji na ujenzi ili kutoka Mifugo Kilosa maji wakati wa kiangazi,"alisema.


Akaasa ili kuwa na ufugaji endelevu na wenye tija wafugaji ni vyema wakamiliki maeneo ya Malisho kisheria ya kuendelea na kufuga kibiashara na hiyo itapunguza migogoro ya matumizi ya ardhi na kuleta amani.


Mwenyekiti wa Chama cha Nyanda za Malisho Tanzania RST Profesa Ismail Selemani alizungumza changamoto na mahitaji yaliyopo ambapo alishauri kuwa ni muhimu Nyanda za Malisho zikasimamiwa kwa maisha ya watanzania na zinachangia kuimarisha usalama wa chakula, Pato la kaya,na kupunguza umaskini.


Aidha Prof. Selemani alipongeza Serikali kupitia Wizara ya Mifugo kwa namna inavyofanya kupanga matumizi Bora ya ardhi na kuongeza maeneo ya machunga na kuyaboresha.


Naye Dk Talik Saleh Suleiman,mkurugenzi mkuu,taasisi ya utafiti wa mifugo Zanzibar alisema kuna fursa za kutengeneza chakula Cha kuku ingawa kuna baadhi ya changamoto za kuagiza chakula Tanzania bara.


Alisema watu wa Zanzibar Wana uwezo wa kuzalisha vyakula vya Mifugo kwa ujumla kwani ni fursa kwao.


Katika hatua nyingine Prof Shemdoe alibainisha kuwa Wizara ipo kwenye mchakati wa kuandaa uanzishwaji wa mamlaka ya Bodi ya Mazao na miundombinu ya Mifugo kwa ajili ya kusimamia masuala ya Sekta ya Mifugo.


Pia alisema Wizara kupitia mradi wa Rangeland Restoration katika Mwaka wa 2023/2024 ilianza utafiti wa mbegu za Malisho ya asili katika Nyanda za Malisho zilizoharibika ambapo yamefanyiwa majaribio ya kuotesha mbegu hizo katika vitalu na matokeo yameonekana kuwa zinaota vizuri.

No comments: