BUNIFU NCHINI ZATAKIWA KUENDELEZWA ZAIDI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 14 April 2025

BUNIFU NCHINI ZATAKIWA KUENDELEZWA ZAIDI

 




Na Lilian Kasenene,Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


BUNIFU zinazovumbuliwa hapa nchini zinapaswa kuendelezwa zaidi kwani uzoefu unaonyesha kuwa nchi nyingi zilizoendelea dunia zimefanya vizuri zaidi kutokana na kuwekeza nguvu kubwa katika kuwezesha bunifu katika nchi zao.


Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uzamili, Tafiti uhaulishaji wa Teknolojia na Ushauri wa kitaalamu kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Profesa Japhet Kashaigili, alisema hayo wakati wa kongamano la Ubunifu lililohusisha wanafunzi kutoka SUA na Chuo Kikuu cha Mzumbe katika wiki ya ubunifu nchini.


Profesa Kashaigili alisema kuna bunifu zimekuwa zikibuniwa na zinazohusiana na teknolojia mbalimbali kwenye masuala ya kuweza kumsaidia hata mkulima wa kawaida namna ya kuweza kupambana na wanyama wahalibifu shambani.


“Ubunifu huu ni kuwaandaa vijana kutoka kwenye nadhalia kwenda kwenye vitendo ambayo ni lengo kuu linalosimamiwa na kuliendelea kama chuo kikuu Sua na hii ni katika kuhakikisha kwamba wanafunzi wanapotoka chuoni wanakuwa wameiva kwenye masuala ya kuendeleza bunivu zao na kuwatoa katika hali ya sasa na kuwapeleka kuwa sehemu ya wigo mpana wa kuweza kuchangia katika maendeleo na kutatua matatizo yaliyopo,”alisema Prof Kashaigili.


Pia alisema kongamano hilo limelenga masuala ya ubunifu unaopelekea uvumbuzi na kwamba kwa sasa wapo wanafunzi waliopo kwenye hatua mbalimbali za masomo,ni kwamba bunifu nyingi za wanafunzi hao zikiendelezwa zina uwezo wa kuwatoa hapo walipo na kuwaendeleza zaidi ndani na nje ya nchi na kuwezesha kuingia kwenye soko la ushindani.


“Bunifu zinatakiwa na hapa tunatakiwa kuzitambua ikiwa ni za viwanda,kilimo, ama teknolojia na sehemu mbalimbali hii itasaidia jamii,lakini lazima tushirikiane na sekata binafsi na huo ndio msingi na muhimili wa maendeleo,”alisema.


Akifungua kongamano hilo Naibu Makamu Mkuu wa Cho Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA, anayeshughulikia Mipango, Fedha na Utawala Profesa Amandusi Mhahilwa aliwataka wasomi kuendelea kujifunza vitu vipya huku wakifanya kazi kwa kushirikiana pamoja na kujiandaa kisaikolojia katika kushughulikia matatizo yanayowazunguka kwemye jamii.


Profesa Mhahilwa alisema katika mafunzo yao ya kawaida nguvu kubwa inayotumika kwa mwanafunzi wa SUA anapofika mwaka wa tatu,nne au wa tano lazima apewe mradi wa kufanya kivitendo ambao utaanza kumuweka katika mazoea.


Alisema “Katika mafunzo ya leo tunachotaka hata akitoka chuoni aendelee na hapa tunawaonyesha wale waliofanikiwa baada ya kutoka hapa,tunachosisitiza kwanza ni kuhakikisha wanakuwa na moyo wa ugunduzi na ushirikiano na watu wengine kwani wanapomaliza wanafanyakazi na watu ila kinachopungua kwao ni kutojiami,”.


Aidha alisema mwanachuo yeyote anayetoka kwenye vyuo ni kuwaandaa kisaikolojia na wanachotegemea ni kuongoza na kukabiliana na shida zinazomzunguka mwanadamu.


Mwanafunzi Asma Soud alisema wamekuwa wakijifunza namna ya kuongeza thamani kwenye bidhaa kabla ya kwenda sokoni huku akitoa wito kwa vijana wenzake kutokaa majumbani na badala yake na kufikilia cha kufanya kwa kutumia fursa wanazozipata na kuwa wabunifu kwa kutumia upawa walionao ndani yao.


Naye mwanafunzi Jesca John alisema kutokana na kuwa na bunifu zao ni kuwasaidia kukuwa kiuchumi,watapunguza wimbi la vijana kukosa ajira mitaani,itawasidia kutombweteka kwa kusubria ajira za serikali ama sekta binafsi.

...........

No comments: