Na Mwandishi Wetu
maipacarusha20@gmail.com
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limekabidhiwa tuzo ya Mdhamini Mkuu kwa kutambua mchango wake katika kufanikisha Maadhimisho ya Kumbukizi ya Miaka 103 ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa, Mwl. Julius K. Nyerere.
Tuzo hiyo imetolewa na Mhe. Dkt. Philip Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kupokelewa na Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, Musa Nassoro Kuji katika hafla iliyofanyika leo Aprili 13, 2025, katika Ukumbi wa Dkt. Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment