MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU TANZANIA (THRDC) WAFANIKISHA DHAMANA YA MWLIMU JOSEPH MUHONIA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday, 12 April 2025

MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU TANZANIA (THRDC) WAFANIKISHA DHAMANA YA MWLIMU JOSEPH MUHONIA

 


Na Mwandishi Wetu 


maipacarusha20@gmail.com 


Leo Tarehe 12/04/2025 Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umefanikisha mchakato wa dhamana ya Mwalimu Joseph Muhonia. Jana Aprili 11, 2025 Mwalimu huyo alipanga kufanya mkutano na waandishi wa habari ili kuzungumzia matatizo yanayowakumba walimu nchini. Kabla ya kufanya mkutano na waandishi wa habari alikamatwa na kufikishwa katika kituo cha Polisi Kati Mwanza. 


THRDC ilimuagiza wakili wake Edwin Hans ambaye yuko Mkoani Mwanza ambaye ameshughulikia mchakato wa dhamana na kufanikiwa kupata dhamana ya Mwalimu Joseph Muhonia. Mwalimu Muhonia alishikiliwa kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko usio halali na ametakiwa kuripoti kituo cha Polisi siku ya Jumatatu Aprili 14, 2025. 


THRDC inatoa wito kwa Jeshi la Polisi kuheshimu haki ya uhuru wa kujieleza ya Mwalimu Joseph Muhonia. Haki hii ipo kwa mujibu wa Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunatoa wito pia kwa Jeshi la Polisi kurejesha simu na vitambulisho vya Mwalimu Muhonia. THRDC inaendelea kufuatilia suala hili kwa ukaribu ili kuhakikisha Mwalimu Muhonia zinazingatiwa. 


No comments: