DKT. KIKWETE AWASILISHA UJUMBE WA RAIS SAMIA KWA SERIKALI YA CONGO BRAZZAVILLE - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 15 April 2025

DKT. KIKWETE AWASILISHA UJUMBE WA RAIS SAMIA KWA SERIKALI YA CONGO BRAZZAVILLE






Na Mwandishi Wetu 


maipacarusha20@gmail.com 


Rais wa Awamu ya Nne na Mjumbe Maalum wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amewasilisha Ujumbe Maalum kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Congo (Congo Brazzaville), Mhe.  COLLINET MAKOSSO Anatole. Mhe. Anatole alipokea ujumbe huo wa maandishi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Congo , Mhe. Denis Sassou Nguesso ambaye alikuwa kijijini kwao kushiriki mazishi ya kaka yake.


Tukio hilo lilifanyika jijini Brazzaville Aprili 14, 2025 na kushuhudiwa na baadhi ya maafisa waandamizi wa nchi zote mbili.


Mhe. Kikwete aliwasilisha pia salamu za Rais Samia ambazo zilielezea umuhimu wa nchi za Afrika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kama njia muhimu kwa bara hilo kujitegemea, hususan katika kipindi hiki ambapo misaada kutoka nchi za magharibi imepungua kwa kiasi kikubwa.

No comments: