UNDP yaridhishwa na MAIPAC ilivyotekeleza mradi uzio chanzo Cha maji Monduli.D - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 9 April 2025

UNDP yaridhishwa na MAIPAC ilivyotekeleza mradi uzio chanzo Cha maji Monduli.D

 





Mwandishi wetu,MAIPAC


maipacarusha20@gmail.com 


Shirika la maendeleo la umoja wa mataifa(UNDP) kupitia programu ya miradi midogo,limeeleza kuridhishwa na utekelezwaji wa mradi wa ujenzi wa uzio wa kulinda chanzo cha maji cha kabambe ambao umefanywa na taasisi ya wanahabari ya kusaidia jamii za pembezoni(MAIPAC)


Mradi huo ni sehemu ya mradi wa MAIPAC wa kulinda na kuhifadhi maarifa  ya asili unaotekelezwa katika kijiji cha Selela wilayani Monduli na Eyasi wilayani Karatu.


Mratibu wa programu ya miradi midogo ya UNDP Faustine Ninga anasema wameridhiahwa na ujenzi wa uzio wa chanzo Cha maji kabambe kinachotegemewa  na wakazi wa vijiji vinne vinavyounda  Kata ya Selela.

"Tumeridhishwa na ujenzi wa uzio wa chanzo hiki Cha Maji hapa kabambe ambacho kinategemewa kwa maji ya kunywa na matumizi ya nyumbani na umwagiliaji shambani na tumeshuhudia jinsi uzio huu unavyodhibiti wanyama waharibifu kuvifikia vyanzo vya Maji." Alisema 

Amewapongeza Maipac kwa kuusimamia vema  mradi huo na kuwashukuru kamati ya Mazingira ya Kijiji Cha Selela kwa kushiriki vema katika ujenzi wa uzio huo.

Akielezea mradi huo Mkurugenzi wa taasisi ya MAIPAC Mussa Juma anasema kuwa wanashukuru UNDP program ya miradi midogo kwa kuwawezesha kufanikisha ujenzi wa uzio wa chanzo hicho Cha Maji.


Mwenyekiti wa mfereji wa maji na mmoja wa wanufaika wanasema kukamilika kwa uzio huo unawapa uhakika wa usalama wa chanzo Cha maji kwani wanyama waharibifu, mifugo na shughuli za kibinadamu kufikia chanzo hicho Cha Maji.


Watendaji wa UNDP na tasisi ya jumuiko la maliasili Tanzania(TNRF) wanatembelea miradi inayofadhiliwa na UNDP kupitia mfuko wa mazingira duninia(GEF) na katika utelelezwaji wa miradi hiyo MAIPAC inakusudia kutoa kitabu cha maarifa ya asili ya jamii ya kimasai,Kidatoga na Kihadzabe katika kulinda na kuhifadhi wa mazingira,vyanzo vya maji na misitu.


Mwisho



No comments: