MWENGE WA UHURU WAZINDUA MACHINJIO YA KISASA YA BILIONI 26 HALMASHAURI YA CHALINZE - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 10 April 2025

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MACHINJIO YA KISASA YA BILIONI 26 HALMASHAURI YA CHALINZE

 






Na Julieth Mkireri, MAIPAC CHALINZE


maipacarusha20@gmail.com 


MWENGE wa Uhuru umekagua mradi wa machinjio ya kisasa uliopo Vigwaza Halmashauri ya Chalinze ambao umetekelezwa kwa gharama ya sh. Biln 26.


Mwenge wa Uhuru leo April 10 unqkimbizwa katika Halmashauri ya Chalinze ukitokea Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha.


Mkurugenzi wa machinjio hiyo Mariam Mnghwani amesema mradi huo una uwezo wa kuchinja ng'ombe 300 mbuzi na kondoo (3000) kwa siku na kwamba una uwezo wa kuhifadhi nyama tani 150 kwa wakati mmoja.


Mariam amesema machinjio hayo kwasasa yanazalisha tani tatu kwa siku na kutoa ajira rasmi 120  na zisizo rasmi na bidhaa za ziada zinazozalishwa ni pamoja na ngozi, damu, mifupa, kwato na pembe.


"Pia Ili kurejesha fadhila kwa Jamii tumewajengea wananchi Zahanati iliyogharimu sh. Miln 180 ambayo itahudumia wana


Amesema lengo la mradi huo nikuzalisha nyama safi, bora na  salama kwa masoko ya ndani na nje ya nchi kujipatia kipato cha fedha za ndani,  zakigeni, kulipa Kodi stahiki na kutoa ajira kwa Jamii kwa kuwapa wafugaji soko la uhakika.


Kwa mujibu wa Mkurugenzi huo Wana Mpango wa kutoa elimu kwa wafugaji wa eneo hilo Ili kuzalisha mifugo yenye ubora kwa masoko ya ndani na nje ya nchi.


Mwenge wa wa Uhuru ukiwa Halmashauri ya Chalinze umekagua, umezindua na kuweka mawe ya Msingi katika miradi ya maendeleo saba yenye thamani ya sh Biln 28.9.


Mwisho

No comments: