Na Lilian Kasenene,Morogoro
maipacarusha20@gamil.com
KAIMU Katibu Wizara ya Afya Dk Saitore Laizer amesema Serikali itaendelea kuwekeza katika sekta ya afya kwa kuhakikisha kuwa wahudumu wa afya wanapata mazingira Bora ya kazi,ikiwa ni pamoja na kuendelea kuboresha miundombinu ya Hospitali, vituo vya afya na Zahanati.
Dk Laizer alitoa wito huo wakati akizungumza katika Jukwaa la wasichana wahitimu wa Elimu ya Uuguzi na Ukunga 257 waliowezeshwa na Shirika la CAMFED, hafla iliyofanyika mkoani Morogoro.
Dk Laizer alisema uboreshaji huo ni ili kuhakikisha huduma za uzazi zinakuwa Bora na zinawafikia wananchi wote hasa walioko maeneo ya vijijini.
"Serikali itaendelea kuhakikisha wahudumu wa afya wanapewa mafunzo ya mara kwa mara ili kuboresha ujuzi wao,hivyo nawahimiza kuchangamkia fursa za mafunzo na kushirikiana na Serikali katika kuboresha huduma hizo za afya nchini,"alisema.
KAIMU Katibu mkuu huyo alilipongeza Shirika hilo la CAMFED Tanzania kwa namna lilivyowezesha na kutoa mchango kwa wasichana hao kupata Elimu ya Uuguzi na Ukunga na kwamba ni mwangaza kwa Kizazi Cha Sasa na kijacho.
Aidha alisema Camfed kama waandaaji wa jukwaa hilo wamefanya na kuonyesha matunda ya uwekezaji katika Elimu ya wasichana na kwamba huo mchango kwa Shirika katika kusaidia Maendeleo endelevu kwenye sekta ya afya nchini na hatimaye kuleta mabadiliko chanya.
"Serikali inatambua mchango wa Camfed na wadau wengine wa Elimu, na hii ni katika kuhakikisha watoto wa kike wanapata fursa sawa za elimu na wanapewa mazingira wezeshi ya kufanikisha ndoto zao,"alisema.
Alisema Elimu waliyopata ni nguvu ya mabadiliko katika maisha yao na jamii kwa ujumla kwani kazi ya Uuguzi na Ukunga ni uti wa mgongo katika sekta ya afya ambayo inahusisha moja kwa moja na ustawi wa mama na mtoto ambayo ni mojawapo ya vipaumbele vya Serikali.
Akawataka kuwa wabunifu na kuendelea kujifunza na huduma wanazotoa zinazingatia viwango vya taaluma na maadili yao,huku akawataka kuwa mabalozi wa mabadiliko katika sekta hiyo.ya afya.
Mratibu wa ufadhili wa Uuguzi na Ukunga ambaye pia ni afisa wa Camfed mkoa wa Tanga Tukaeje Mzeru alisema Camfed Mwaka 2021 ilipata ufadhili kuweza kusaidia wasichana wanaotoka katika mazingira hatarishi wanaosoma masomo ya Uuguzi na Ukunga kwa programu ya miaka minne ambapo nchi za Tanzania na Ghana zilifanikiwa kupata ufadhiri huo.
Mzeru alisema leongo la ufadhili huo ni kuongeza idadi ya wafanyakazi wa afya hasa katika maeneo ya vijijini ili kuboresha upatikanaji wa huduma za afya na kupunguza vifo vya mama na watoto wakati wa ujauzitona kujigufungua.
"Camfed kwa kushirilikiana Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya ilikubaliana vyuo vya afya 20 vitumike kufundushia na programu hiyo ilipagwa kuwafikia wasichana 280 nchini Tanzania kwa kuwagharamia ada za masomo, malazi, chakula, vifaa vya kujifunzia, na usafiri ili kuhakikisha wanajikimu bila ya usumbufu wa kifedha.
Alisema hadi sasa wasichana 298 wamefikiwa katika vyuo vya Serikali 20 ambapo mbali na kunufaika na masomo ya afya pia walipata mafunzo ya ujasiliamali na Biashara ili waweze kujiajili pindi watakapokuwa na changamoto za ajira na hata kuweza kufungua biashara kwa kutumia taaluma yao.
Mratibu huyo alisema kiasi cha sh bilioni 4,239,905,035.19 zimetumika kwa ajili ya ufadhili wa wanafunzu 298,na wanafunzi 257 ndo wamefanya mtihani na kufahulu huku wanafunzu 16 wakiendelea na masomo yao baada ya kurudia baadhi ya Moduli kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya kupata ujauzito,kubadilisha kada ,ugonjwa wa muda mrefu, matatizo ya kifamilia na kuahirisha masomo.
Mkurugenzi Camfed Nasikiwa Duke alisema Camfed ina malengo ya kufikia na kufadhili mabinti 2,000 na kwamba msukumo wa kufadhili mabinti hao na mipango yao ya kuongeza wahitaji hao kuhakikisha jamii za pembezoni zinafikiwa kwa haraka hasa kwenye suala la afya..
Muuguzi Janeth Charles alisema wao wamejioanga kwenda kuhudumia jamii kutokana na yake waliojifunza
Katika hatua nyingine kaimu katibu mkuu Wizara ya Afya Dk Laizer alitoa onyo kwa wahudumu wa afya nchini kuacha kuomba na kupokea fedha mara baada ya kutoa huduma ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi.
Mwisho..
No comments:
Post a Comment